Watumish wa Halimashauri ya Manispaa ya Iringa wameshauriwa kujenga mazoea ya kuandika usia binafsi au kwa wanandoa ili kuepusha migogoro ya kifamilia pindi mmoja anapofariki.
Rai hiyo imetolewa leo tarehe 22.5.2023 katika ukumbi wa mikutano Mamispaa na ndugu Magoti Afisa wa Rita alipokuwa akizungumza na watumishi wa kada mbalimbali kutoka ofisi kuu Manispaa ya Iringa.
Aidha Magoti amesema, " ni vizuri tuwe na mazoea ya kuandika usia ili pindi Mume au Mke mmoja anapofariki, kusiwe na migogoro ya mali au ya watoto."
"Kuna dhana imejengeka kuwa kuandika usia ni kujichuria( mkosi) kifo, kitu ambacho si kweli, kwani kufa ni lazima na kila mtu atakufa."
Aidha Magoti aliwataka watumishi kuhakikisha wanafika Rita ili waweze kupatiwa vyeti mbalimbali haswa vya kuzaliwa, ndoa na vifo.
"Nawaomba msizembee kila mmoja anapaswa kuhakikisha anaenda Rita kupata cheti cha kuzaliwa pamoja na vya watoto wenu, pia wanandoa msiishi kwa mazoea fungeni ndoa rasmi iwe ya kiislam, kikristu au ya kiserikakali ili muweze kupata vyeti vya ndoa halisi vinavyotambulika kisheria."
Mkiwa na nyaraka hizi inakua ni rahisi kwa mtu kufatilia madai mbalimbali kama vile mirathi, kupata haki ya kurithi n.k
Mwisho aliwatoa hofu watumishi kwa kuwaelezea kuwa gharama za kuandika na kuhifadhi usia sio kubwa kwani inampasa mtu kuwa na kiasi cha shilingi 40,000/- tu kwa miaka yote atakayotunza.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa ndugu Charles Mwaitege alishukuru kwa elimu iliyotolewa na kusema anaimani watumishi wamepata faida kubwa kupitia somo hilo na kuwataka wayazingatie na kuyafanyiakazi kwa faida ya baadae.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa