Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa Iringa amabaye pia ndie Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Mhe. Ibrahim Ally Ngwada ametoa hoja binafsi kuhusu ukarabati wa majengo yaliyochakaa katikati ya mji.
Hoja hiyo ameitoa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani kujadili taarifa ya robo ya kwanza kuanzia Julai mpka Septemba, 2023, uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa mwanzon mwa wiki hii.
Ngwada ameeleza kuwa katikati ya mji Majengo mengi ni mabovu na chakavu sana na yamekua hatarishi kwa wakazi wake, lakini vilevile yanapelekea mji wetu kuonekana mchafu na hii yote inasababishwa na sheria za mipango miji inayomtaka mkazi yeyote anayetaka kufanya ukarabati wa nyumba yake iliyopo katikati ya mji sharti ajenge ghorofa.
“watu wengi wamekua wakitamani kufanya ukarabati majengo yao ili yawe ya kisasa lakini wanashindwa kutokana na gharama za kujenga ghorofa kama sheria inavowataka, lakini ukiangalia wapo teyari kujenga nyumba za chini na za kisasa, sasa kwanini tusiwaruhusu wafanye ukarabati kwa sasa na wakati ukifika wa kujenga maghorofa tutakaa chini tena tuangalie upya.” Amesema Ngwada.
Najua tunatamani Mkoa wetu uwe Jiji na tunaelekea huko, lakini siyo kweli kwamba maghorofa ndiyo yanaleta kigezo cha sisi kuwa jiji. Lengo la hoja hii ni kuufanya mji uwe safi na uvutie lakini pia ni kuepusha madhara, kwani majengo mengi ni mabovu na yanaweza kuanguka na kusababisha vifo kwa watu.
Aidha Diwani wa kata ya Mkimbizi na Mjumbe wa Baraza hilo Mhe. Eliud Mvela alipingana na hoja hiyo kwa kueleza kuwa wawekazaji watakuja na wataubadilsha mji kwa kujenga maghorofa na siyo lazima wawe wazawa kwani hata Kariakoo ya Dar es salaam haijajengwa na wazawa bali wageni.
“mheshimiwa Mwenyekiti, Kariakoo mnayoiona ile imejengwa na Wakinga, Wachagga na wageni wengine na wala siyo Wazaramo(wazawa), hivyo hata sisi tuwe naimani ya kuwa wawekezaji watakuja na wataporomosha maghorofa hapa na mji wetu utapendeza na kuwa Jiji kama tunavyotamani.” Amesema Diwani Mvela.
Wajumbe wengine walipopata nafasi ya kuchangia hoja hiyo, waliiunga mkono kwa kuona mji haupendezi kutokana na uchakavu wa majengo na wamiliki hawana uwezo wa kuyavunja na kujenga ghorofa, lakini wapo teyari kujenga nyumba za chini na za kisasa, hivyo wakatoa rai juu ya hoja hiyo kuwa utengwe muda maalum wa kujadili hoja hiyo.
Huku Mkurugezi wa Manispaa Iringa Ndugu Kastori Msigala alishauri hoja hiyo ipelekwe ikaanzie kwenye kikao cha menejimenti ili kuwepo na ushauri wa kitaalamu na baadae kujadiliwa katika vikao vya maamuzi ya juu ya Halmashauri.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa