Wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Machinga Manispaa ya Iringa wamepiga kelele za shangwe vifijo na nderemo mara baada ya kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan katika ziara yake Mkoani Iringa baada ya kusema anatambua mahitaji yao ni eneo la kufanyia biashara hivyo Serikali ya awamu ya sita itahakikisha wanapata maeneo hayo kwa kutoa zaidi ya shilingi milioni 700 zitakazoendeleza ujenzi katika eneo la soko la Mlandege na kuhakikisha wanapata sehemu nzuri ya kufanyia biashara bila bughudha yeyote
Mhe.Samia ameyasema hayo katika viwanja vya Samora tarehe 12 Agosti wakati akihututubua maelfu ya wanachi waliofika kumsikiliza
Mhe Samia pia amesema anatambua changamoto ya wanachi wa Manispaa kuwa ni daraja kutoka Isakalilo kuunganisha Kitwiru hivyo Serikali itagharamia ujenzi wa daraja hilo ili kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi ambao wamepata adha kwa muda mrefu.
Mhe Samia ambayea aliambatana na baadhi ya Mawaziri,ma naibu waziri na viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali waliokuwa tayari kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusiana na utekelezaji wa shughuli katika wizara zao
Awali akizungumza waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu amesema Serikali inamikakati ya kuboresha huduma za afya kwa kununua vifaa tiba pamoja na kuajiri wataalamu watakao toa huduma katika vituo vya afya,,zahanati na Hospitali za wilaya ili kupunguza adha kwa wananchi
Pia Mwalimu amesema wanampango wa kununua magari ya kusafirishia wagonjwa (Ambulance) kila wilaya ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake Waziri wa Kilimo ndugu Bashe amesema Serikali imepunguza gharama za pembejeo ili kutoa unafuu kwa wakulima ambapo bei hizo zimepungua kwa kiasi kikubwa ambacho Serikali imezichua gharama hizo.
Amesema mbolea zote za kupandia ambazo zilikuwa zikiuzwa sh.120000 kuanzia tarehe 15/8/2022 wananchi watanunua kwa bei ya sh 70,000 tu
ZIara ya Mhe.Samia Mkoani Iringa imekuwa ya mafanikio makubwa kwa wanachi kwani imetoa utatuzi wa changamoto za muda mrefu ambazo zimekuwa zikiwakabili kama miundo mbinu,upubgufu wa watumishi katika sekta mbali mbali,ukosefu wa vifaa tiba.
Aidha akihitimisha ziara hiyo katika Tarafa ya Isimani Iringa vijijini mhe Samia aliwataka wanachi kutokuwanywesha ulanzi watoto na badala yake wawanyeshe maziwa ili wawe na afya njema.
'Mkoa wa Iringa ni wazalishaji wazuri sana wa chakula lakini cha kushangaza watoto wengi wana udumavu,jamani msiwanyweshe ulanzi watoto wanyesheni maziwa.alisema Samia'
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa