Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Iringa limemchagua Mhe. Juli Sawani kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa katika Uchaguzi uliofanyika kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Mwaka Jumatatu 09, Septemba 2024 katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa .
Akiongoza mchakato wa uchaguzi huo Meya wa Manispaa ya Iringa, Mhe. Ibrahim Ngwada amesema kuwa uchaguzi huo unazingatia kanuni na taratibu za uongozi wa Baraza hilo ambapo hushirikisha wajumbe (Madiwani) kupiga kura na kumchagua Naibu Meya na Uteuzi wa wajumbe wa kamati za kudumu ambao wataongoza kwa muhula wa Mwaka Moja (2024/25) mpaka kufikia uchaguzi mkuu
ujao wa Mwaka 2025.
Awali, Uchaguzi huo ulifanywa na wajumbe 21 ambao walipiga kura za Ndiyo na Hapana ambapo madiwani wote 21 walimpigia kura za Ndiyo Mheshimiwa Sawani na kumpa ushindi usio na mpinzani.
Akiongea baada ya ushindi huo, Mhe. Sawani ametoa shukrani za dhati kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa na Madiwani kwa ujumla kwa ushirikiano waliounyesha katika muda wote ambao wamefanya kazi na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kiujumla kwa kuendelea kumuamini na kumpigia kura hivyo kuahidi kushirikiana nao katika kuwatumikia wananchi wa Iringa kwa lengo la kuwaletea maendeleo.
"Nawashukuru sana Waheshimiwa
Madiwani, Mkurugenzi na Wataalamu kwa ushirikiano mliounesha kwa mwaka uliopita. Nawashukuru pia kwa kuniamini na kunichagua kuwa kiongozi wenu tena, Naahidi kushirikiana nanyi ili tukamilishe na kutekeleza ahadi tulizotoa kwa wananchi,pia naahidi tutashirikiana na Mstahiki Meya wa Manispaa katika kumshauri mambo mbalimbali ya maendeleo na yanayogusa kutatua kero na matatizo ya wananchi wa Manispaa kiujumla". Amesema Sawani.
Aidha, kikao hicho kiliambatana na uundaji wa Kamati za Kudumu za Halmashauri pamoja na uchaguzi wa Wenyeviti wa Kamati hizo ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya kudhibiti ukimwi kwa mujibu wa kanuni ni Naibu Meya ambaye ni Ndg. Juli Sawani, Kamati ya Mipangomiji na Mazingira ilimchagua Mhe.Hamid Mbata, Mwenyekiti
aliyechaguliwa kwenye Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu ni Mhe. Eliud Mvela huku Kamati ya Maadili ilimchagua Mhe. Mahadhi Hepautwa, na Kamati ya Mfuko wa Jimbo imewateua Waheshimiwa Kenyata Likotiko na Hellen Machibya. Kamati ya Bodi ya ajira aliyeteuliwa ni Mhe. Hamid Mbata
Wajumbe wengineo walioteuliwa ni wawakilishi wa ALAT Mkoa ambao ni Mhe. Juli Sawani na Pascalina Lweve. Mwakilishi aliyeteuliwa kwenye Bodi ya IRUWASA ni Mhe. Thadeus Tenga Wajumbe wawakilishi kwa Kamati ya kugawa Ardhi ni Mhe. Hellen Machibya na Amri Kalinga.,Kamati ya Fedha na uongozi itakuwa chini ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa,Naibu Meya, wenyeviti wa kamati zote pamoja na Mhe.Amri Kalinga na Mhe.Christina Ngohani wajumbe wa kuteuliwa
Akifunga kikao hicho Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada amewaasa Madiwani, Mkurugenzi na Wataalamu wa Manispaa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuongeza mapato ya Halmashauri na hatimaye kuweza kukamilisha miradi ya Manispaa kwa nia ya kuwaletea maendeleo wananchi na Taifa kwa ujumla.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa