Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa imeipongeza Halmashari ya Manispaa ya Iringa kwa kazi nzuri ya usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2017-2018
Pongezi hizo zilitolewa wakati wa ziara ya Sekretarieti ya Mkoa ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Manispaa ya Iringa na kuitaka kuendelea na juhudi za utekelezaji wa miradi hiyo ili kuleta tija
Aidha miradi iliyotembelewa ni pamoja na kukagua ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari ya wasichana Iringa, mabweni na madarasa Shule ya Msingi Ipogolo, ujenzi wa madarasa Shule ya Sekondari Kihesa , ujenzi wa madarasa Shule ya Sekondari Mkwawa, ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Kigonzile, ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule ya msingi Njia panda, ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Mtwivila, ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Mshindo, ujenzi wa nyumba ya mwalimu Shule ya msingi Mlangali, ujenzi wa Zahanati ya Itamba pamoja na ujenzi wa Soko la Mlandege.
Mbali na hayo Sekretarieti imewataka wakandarasi wa Miradi hiyo kukamilisha kazi hizo kwa wakati ili miradi mengine ya maendeleo iendelee.
Ziara hiyo ya sekretarieti ya Mkoa ilikuwa na lengo la kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inakuwa katika hatua nzuri ya kukamilika.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa