Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jimbo la Iringa Mjini Ndugu, Omary Mkangama amefanya Semina fupi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Serikali za Mitaa tarehe 4/10/2019 katika Ukumbi wa Community Center lengo likiwa ni kuwakumbusha Majukumu yao kama vile kujua sifa za Waandikishaji, sifa za kujiandikisha kupiga Kura pamoja na Sheria na Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Aidha, amewaasa kuwa waadilifu na waaminifu katika Kazi ya Uchaguzi ili kuepusha vurugu siku ya uchaguzi Pia, Hakimu Ndugu, Ritha Protas Rutakyamirwa amewapisha Wasimamizi Wasaidizi wa uchaguzi.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa