Shule mpya ya Msingi ya Uyole iliyopo Kata ya Kitwiru imefanyiwa dua / maombi na viongozi wa dini kutokana na radi iliyopiga katika shule hiyo na kujeruhi wanafunzi 11 na mwalimu mmoja wakiwa darasani.
Maombi hayo yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Chama Cha Mapindizi (CCM) huku wakiongozwa na Mstahiki Meya Mhe. Ibrahim Ngwada aliyeambatana na Naibu Meya Mhe. Juli Sawani na Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi (CCM) pamoja na viongozi wa Kata.
Aidha Mstahiki Meya amewashukuru wazazi na wananchi wote waliojitokeza na kuwasihi waendelee na umoja huo kwani tatizo ni la kwetu wote na nivizuri tukawa tunashikamana kwa pamoja.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego akizungumza kwanjia ya simu amemshukuru Mstahiki Meya, Viongozi wote pamoja na wananchi wote kwa kujitoa na kutoa pole kwa wanafunzi wote waliopata madhara kwa namna moja au nyingine kutokana na radi.
“Natoa pole kwa wanafunzi walioathirika na radi pamoja na wanafunzi wote kwa mshtuko waliopata” Amesema Dendego
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa