Timu ya ufatiliaji kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Lengo la ziara hiyo iliyofanyika tarehe 7/7/2021 ni kuona maendeleo ya miradi inayojengwa kwa kutumia fedha kutoka Serikali kuu na mfuko wa jimbo kwani ni utaratibu wa kawaida kukagua miradi hiyo kila mwisho wa mwaka wa fedha
Sweetbert Masato ni Mchumi Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango kutoka Ofisi ya Rais ametoa rai kwa Mkurugenzi wa Manispaa kusimamia kwa kufuata taratibu/ mwongozo wa ujenzi wa miradi hiyo ili iweze kujengwa kwa kiwango kinachotakiwa kulingana na fedha zilizotolewa ili ilete tija kwa kutatua changamoto za wananchi
'Ni muhimu Halmashauri ikafuata mwongozo uliotolewa na Wizara husika kwa ajili ya ujenzi wa miradi kwani kuna mapungufu madogo yamejitokeza kwenye baadhi ya majengo natoa maelekezo yarekebishwe mara moja na kwa miradi iliyo nyuma ya wakati naagiza Mkurugenzi usimamie hilo ili miradi yote ikamilike kwa wakati.Alisema Masato'
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Mkimbizi,Shule ya Msingi Ilala, shule ya Sekondari ya Mlamke, Umaliziaji na ujenzi wa Zahanati ya Itamba na machinjio ya kisasa Ngelewala
Omary Mkangama ni kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ameishukuru timu hiyo kwa ukaguzi wa miradi na kupokea maelekezo yote yaliyotolewa pia ameahidi kuyafanyia kazi kwa haraka kwa manufaa ya wananchi.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa