Kaimu Mkurugenzi wa mfuko wa kunusuru kaya maskini (TASAF) Makao Makuu Bwana. Paulo Kijazi amefungua mafunzo ya kujenga uelewa kuhusu kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya (TASAF) na uhakiki wa kaya kwa wakuu wa Idara na wawezeshaji ngazi ya Halmashauri Manispaa ya Iringa.
Aidha mafunzo hayo ya siku mbili yameanza leo katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa yakiwa na lengo la kuziwezesha kaya za walengwa katika kutumia fursa za kuongeza kipato, huduma za jamii na uchumi pamoja na kuwekeza katika kuendeleza watoto wao.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Hamid Njovu amewataka wanasemina kuzingatia mafunzo na kuhakikisha wanafuata vigezo vilivyowekwa ili kuwapata wanufaika waliokusudiwa.
Njovu anesema wanufaika watakao patikana wapewe elimu ya matumizi sahihi ya fedha wanazopata ili ziwasaidie kuwaletea maendeleo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa