Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndugu Hamid Njovu amekabidhiwa kombe la ushindi wa kwanza kwa timu ya volleyball Manispaa ya Iringa iliyoshiriki mashindano ya volleyball kwa taasisi za serikali nyanda za juu kusini, yaliyofanyika jijini mbeya.
Akizungumza wakati wa kukabidhi kombe hilo Kepteni wa timu ya volleyball Manispaa Iringa Ndugu Joseph Milinga amesema, imewapa faraja kwa kupokelewa na kuthaminiwa na Mkurugenzi wa Manispaa pamoja na Timu ya menejimenti, jambo ambalo limewapa moyo na kuahidi kuleta tena kombe mwakani.
Aidha Kapteni amesema changamoto wanazokutana nazo ni pamoja na ukosefu wa uwanja wa kufanyia mazoezi, hivyo kumuomba Mkurugenzi wa Manispaa kuwapatia eneo la kudumu ambalo litakua la Manispaa ili waweze kufanya mazoezi bila kusumbuliwa.
Akipokea kombe hilo Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndugu Hamid Njovu amesema, amefarijika sana baada ya timu kurudi na kombe hivyo kuwaomba watumishi kila idara kuitendea haki idara zao kwa kuonyesha uhai wa idara na kubuni shughuli za kufanya ambazo ameahidi kuzisaidia kulingana na bajeti.
“Hongereni sana kwa kupata ushindi ,kila idara na sekta ikija na mikakati inayotekelezeka naahidi kuisaidia.”
Timu ya volleyball Manispaa ya Iringa ilishiriki michezo ya kusini ambayo ilikua na wachezaji 10 chini ya kepteni wao Joseph Milinga.ambapo walishindana na timu mbalimbali za nyanda za juu kusini ikiwemo timu ya kutoka Ruvuma, Njombe, Lindi na Rukwa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa