Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Innocent Bashungwa amewataka Maafisa habari kuhabarisha jamii namna Serikali ya Awamu ya sita inavyotoa fedha za miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha mhe Bashungwa amewataka maafisa habari kuzingatia weledi,ubunifu na jitihada katika kutekeleza majukumu yao ili jamii iweze kunufaika kwa kupata taarifa sahihi na kwa wakati.
Mhe Bashungwa ameyasema hayo katika mkutano uliofanyika leo Julai 2 katika ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakati alipokutana na maafisa habari wa Mikoa,Halmashauri na Taasisi zilizopo chini ya ofisi ya Rais TAMISEMI.
Mhe.Bashungwa amesema Maafisa habari wanajukumu kubwa la kuisemea vizuri Serikali na kuitetea kutokana na mambo ya upotoshaji yanayofanywa katika mitandao ya kijamii na watu wasio Itakia mema nchi yetu.
Aidha mhe.Bashungwa amewataka wakurugenzi na MakatibuTawala wa Mikoa kuhakikisha kitengo cha Mawasiliano Serikalini kinakuwa na vifaa vya kutosha ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri.
Awali akiongea katika Mkutano huo Msemaji Mkuu wa Serikali ndugu Gerson Msigwa amewataka Maafisa Habari kutumia fursa hiyo ya mkutano huo kijipanga na kufanya maboresho ya utendaji kazi wao huku akiwaasa kuwa changamoto walizonazo zisizoroteshe utendaji wao wa kazi na badala yake watimize wajibu wao kwa kufanya kazi kwa bidii ili wanachi wapate taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo na shughuli zingine zinazofanywa na taasisi zao na kusema kuwa wao ni daraja kati ya Serikali na wanachi.
Dr.Charles Msonde ni Kaimu katibu Mkuu TAMISEMI anasema wanatambua Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kinachangamoto nyingi hivyo ameahidi kuzifanyia kazi mara moja ili kuhakikisha maafisa Habari wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.
Katika mkutano huo mada mbali mbali zilitolewa ikiwepo Uanzishwaji wa Kitengo cha Mawasiliqno Serikalini,utekelezaji wa miundombinu ya Afya,utekelezaji wa miradi ya Elimu,Sura ya bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ni zingine .
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa