Mkuuwa Mkoa wa Iringa, Mheshimiwa Halima Dendego amewataka viongozi wa Halmashauriya Manispaa ya Iringa kuhakikisha ajenda ya ukatili wa kijinsia inakuwa ajendaya kudumu katika vikao vyote na mikutano ya Baraza la madiwani ili kutatuatatizo hilo katika Mkoa.
Mkuuwa Mkoa amesema hayo katika Kongamano la Kupinga matukio ya Ukatili wa Kijinsiamkoani Iringa lililoandaliwa na Diwani viti maalum Mhe. Dorah Nziku katikaUkumbi uliopo Soko la Mlandege likiwa na kauli mbiu isemayo "Iringa BilaUkatili Inawezekana".
“Nimpongeze Mheshimiwa Diwani kwa kuandaa kongamano hili kwakuwa litasaidia kupunguzamatukio ya ukatili wa kijinsia, hivyo nawaagiza viongozi wa Manispaa ajenda hiiiwe ni ajenda ya kudumu katika vikao vyote pamoja na mikutano ya madiwaniitusaidie kupata njia ya kutatua hili” Amesema Mhe. Dendego
Diwani viti maalum Mhe. Dorah Nziku amesema lengo la Kongamano hilo ni kupeana elimuzaidi na kuwaleta pamoja wanawake na wanaume katika mapambano ya kutokomezaUkatili wa kijinsia mkoani Iringa ikiwa ni moja ya hatua ya kuelekeamaadhimisho ya siku 16 za Kupinga Ukatili wa kijinsia.
"NimeandaaKongamano hili kwasababu nimeguswa na kuumizwa na vitendo vinavyoendelea katikaMkoa huu, zamani walisema watoto wetu wa kike tuwalinde sana, lakini sasa hivihata watoto wa kiume tuwalinde sana, kwasababu watoto wa kiume wanalawitiwamno" Amesema Dorah
Kongamanohilo limeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego kuhudhuriwa na WanawakeMkoani humo kwa kushirikiana na Umoja wa Wanawake Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoawa Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa