182 WAMERIPOTI KUFANYIWA UKATILI
Imeelezwa kuwa ulevi kupindukia,Imani potofu,Kulegea kwa malezi ya watoto vinachangia kwa kiasi kikubwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto Mkoani Iringa.
Hayo yamebainika leo tarehe 26/11/2022 katika kongamano la uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kimkoa lililofanyika katika ukumbi wa siasa na kilimo uliopo Manispaa ya Iringa
Akifungua kongamano hilo
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Halima Dendego amesema Iringa bila ukatili wa kijinsia inawezekana ikiwa kila mmoja wetu atatimiza wajibu wake ipasavyo.
Mhe.Dendego amelitaka Jeshi la polisi katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kuweka kipaumbele cha kukabiliana na matukio hayo katika upelelezi ili kuwezesha mahakama kutoa hukumu haraka
Aidha Mhe.Dendego ameyataka mabaraza ya watoto Mkoa wa Iringa yapatayo 1433, club za watoto 341,kamati za malezi 207,wakuuu wa Wilaya,Wakurugenzi na Maafisa watendaji kuzuia matukio hayo kwani yanaharibu nguvu kazi ya Taifa na kupoteza ndoto za watoto hao.
'Naagiza kila Halmashauri kwenda kutoa Elimu kwenye Mitaa,Kata na Vijijini Mashuleni na vyuoni wakuu wa Wilaya Wakurugenzi,na watendaji wa Kata hakikisheni mnatoa elimu ya masuala ya ukatili ili wananchi wawe na uelewa mpana kuhusu masuala hayo alisema Dendego'
Awali akisoma risala ya uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na watoto Mkoa wa Ironga Bi.Tiniel Mbaga Afisa Ustawi wa Jamii Manisaa ya Iringa amesema juhudi za kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia zimekuwa zikifanywa na Halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile; Taasisi za umma,Mashirika yasiyo ya kiserikali,Taasisi za dini,vyombo vya habari,vyama vya Siasa na viongozi mbalimbali,vyuo vikuu,vyuo vya kati na makampuni ya watu binafsi.
Mbaga amesema juhudi hizo zimekuwa zikilenga kupunguza matukio ya ukatili kwa kuzuia vitendo vya ukatili visitokee na kuitikia pale vinapotokea.
Pamoja na jitijada hizo bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali wanaposhughulikia masuala ya ukatili kama vile;baadhi ya wananchi kutokuwa na ushirikiano wa kutosha katika kushughulikia mashauri ya ukatili hasa watendaji wa makosa wanapokuwa ni ndugu wa karibu,kesi za ukatili kuchukua muda mrefu mahakamani jambo ambalo linatoa mwanya wa maridhiano baina ya pande mbili na kupelekea kesi kuharibika.
Akisoma ripoti ya matukio ya ukatili ya Mkoa mbele ya mgeni rasmi,Mkaguzi Msaidizi ndg.Paul Bundala amesema matukio 182 ya ubakaji yameripotiwa kwa kipindi cha januari hadi Oktoba mwaka 2022 sawa na asilimia 47 miongoni mwa matukio 384.
Aidha amesema kwa upande wa takwimu za Kitaifa jumla ya matukio 29,373 ya ukatili yaliripotiwa Mwaka 2021 yakihusisha ubakaji,ulawiti, ngono na wanafunzi huku Mikoa ya Arusha,Dare es salaam,Tanga na Rukwa ikiongoza kwa matukio hayo ya ukatili.
Siku 16 za kupinga ukatili huadhimishwa Novemba 25 hadi Disemba 10 kila mwaka.kauli mbiu ya mwaka huu inasema 'KILA UHAI UNA THAMANI.TOKOMEZA MAUAJI NA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO'
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa