Muungano wa vyama vya Ushirika vya akiba na mikopo Tanzania Tanzania umewakutanisha ma meneja 70 wa vyama mbalimbali vya SACCOS kutokea maeneo tofauti nchini katika mkutano wa tatu wa pamoja wa kujadili masuala yanayohusu vyama vyao pamoja na kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi
Mkutano huo utakaotumia siku nne, umeanza leo, Machi 15. 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Mount Rayal, mkoani Iringa kikiwa na ajenda mbalimbali pamoja na kuwataka viongozi hao kuwa waadilifu na waminifu katika kutekeleza majukumu yao
Akizungumza Ndugu, Hassani Mnyone, Mtendaji Mkuu wa Muungano wa vyama na ushirika vya akiba na mikopo Tanzania (SACCOS) amesema, ajenda zitakazojadiliwa ni pamoja na kuzungumzia mwenendo soko la huduma za kifedha linavyokwenda na kuzitazama fursa zilizopo, kuzitambua changamoto wanazowapata na kukabiliana nazo, masuala ya uongozi, pamoja na uboreshwaji wa mifumo ya Tehama itakayosaidia kurahisisha utoaji wa huduma zao
Hata hivyo Ndg, Hassani ameongezea kwa kusema baada ya kumaliza mkutano wao, watapata fursa za kutembelea maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Iringa katika kutoa elimu ya ushiriki kwa vijana mbalimbali wa bodaboda na kutoa zawadi pamoja na kufanya utalii mdogo utakaoweka alama ya kiuchumi ya ujio wao mkoani hapa
“hata hivyo, tutatembelea kituo cha watoto ambayo ni sehemu yetu ya utekelezaji wa msingi namba 7 wa ushiriki unaosisitiza kuhusu kuijali jamii” alihitimisha kwa kusema hayo Ndugu. Hassani
Kwa upande wake Ndugu. Bosco Simba Meneja wa SACCOS ya walimu Wilaya ya Moshi vijijini Mkoani Kilimanjaro ameitaja changamoto ya Tehama kama ni moja ya kikwazo katika uendeshwaji wa vyama vingi vya SACCOS na hivyo kwasasa wamejipanga kuwekeza na kuimarisha mifumo ya Tehama ili kurahisisha utolewaji wa huduma kwa wanachama wao
Hata hivyo Ndugu. Bosco ameishukuru serikali kwa uwekaji wa mifumo mipya, sheria, sera na kanuni pendwa zenye kuongoza vyama vyao kwa kuzifanya ziwe bora zaidi na zenye kuaminiwa na jamii na amesema utoaji wao wa elimu umeleta tija kwa wananchi kuwafanya wajifunze, waelewe na wajiunge katika vyama hivyo
Vilevile ameongezea kwa kusema katika kupunguza matukio ya ubadhilifu wa pesa na katika vyama vyao, wamehakikisha wameendelea kukagua na kujiridhisha kwa viongozi (Mameneja) wanaosimamia vyama hivyo kuwa wanavigezo na ni waadilifu katika kazi hali inayopelekea kuzifanya taasisi zao kuwa zenye kuaminiwa na watu na kuwa na utendaji bora
Mwisho Ndg. Bosco amezitaja SCCULT na Tume ya maendeleo na ushirika (TDCD) ndio taasisi ambazo huzipelekea malalamiko na changamoto zao kwa utatuzi ili kuboresha huduma wanazozifanya
Nae Bi. Elvera Mdee, Meneja wa chama cha ushirika wa akiba na mikopo Samekaya cha Mkoani Kilimanjaro, akiwa mjumbe katika mkutano huo amesema vikao hivyo vinawasaidia kwa kupeana uzoefu, na tangu kuanza kukutana kwao kumesaidia kupungua hali ya kufa kwa vyama ukilinganisha na mwanzoni lakini pia imewapa fursa za kukutana na wataalamu mbalimbali ikiwemo wataalamu wa masuala ya uwekezaji wwkiwapatia elimu ya namna wanavyoweza kuwekeza na kupata faida katika vyama vyao na mwisho amewaomba wananchi kuendelea kuviamini na vyama vyao na kuziamiini huduma zoa na wanaweza kujiunga.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa