Mkuu wa Wilaya ya Iringa Komredi Kheri James amekutana na Wakuu wa Shule na kuwapongeza kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya iliyopelekea matokeo mazuri ya Kidato cha Sita 2024 katika Wilaya na Mkoa kwa ujumla.
Akizungumza na walimu hao katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo akiwa ameambatana na Wakurugenzi wa Halmashauri, Komredi Kheri amesema kuwa kutokana na Serikali kufanya uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Elimu ndio jambo pekee lililopelekea matokeo kuwa mazuri kwani kwasasa Serikali imeboresha miundombinu na kujenga madarasa mapya, pia kuongeza Walimu kwenye Shule na kupandisha madaja kwa walimu
Aidha Kheri amesema kuwa kutokana na matokeo haya mazuri sasa ifike wakati kila mwananchi ahakikishe anakuwa na jukumu la kuhakikisha wanafunzi wanapata Elimu Bora ili kuhakikisha tunatokomeza ujinga katika Taifa letu
Aidha Komredi Kheri amewaagiza Viongozi wa Kata na Kijiji kuweka Ajenda ya elimu kuwa ni ajenda ya kudumu katika vikao vyao na wananchi, huku akiwaagiza Wakuu wa Shule kusimamia fedha zote zinazotolewa na Serikali kwa kuhakikisha miradi inakamilika na inaendana na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali
Kwa niaba ya Wakurugenzi wa Halmashauri akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wamewapongeza walimu hao kwa uchapakazi wao mkubwa wanaoufanya.
Wakizungumza mara baada ya Kikao hicho baadhi ya Wakuu wa Shule wamesema kuwa siri kubwa ya Shule kupata matokeo mazuri kwanza ni miundombinu bora iliyowekwa kwenye shule hizo inayowafanya wanafunzi hao kusoma kwa utulivu na pili ni nidhamu ya wanafunzi, pia wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu na kupandisha madaraja kwa baadhi ya walimu kumekuwa chachu ya utendaji kazi.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa