Vijana wanamichezo Mkoani Iringa wameaswa kuendelea kujituma zaidi na kuonesha nidhamu katika michezo wakiwa katika maandalizi ya kwenda kushiriki mashindano ya UMISETA kitaifa
Hayo yamesemwa Agasti 4.2022 na Mhe. Rita Kabati, Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa ambaye ni mgeni rasmi katika kufunga mashindano ya UMISETA ngazi ya Mkoa yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Lugalo
Hata hivyo Mhe. Rita Kabati ametoa ahadi kwa vijana hao kuwatembelea zaidi wakati wa kambi kwa kuwapa hamasa na ameahidi kutoa zawadi nono kwa timu zitakazorudi na ushindi wa makombe katika ushiriki wao
Kwa upande wake Ndg. Gelvas Simbeye ambaye ni kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Iringa amesema jumla ya wanamichezo 120 ndio wamechaguliwa kwenda kushiriki katika mashindano ya UMISETA kitaifa wakiwakilisha Mkoa wa Iringa huku akiwa na matumaini ya kurudi na ushindi katika makundi mbalimbali ya michezo ambayo watashiriki kitaifa Mkoni Tabora ambayo yataanza tarehe 9 mpaka tarehe 20 mwezi Agasti mwaka huu.
Aidha Simbeye amesema michezo watakayoshriki ni Mpira wa miguu, kwa wavulana na wasichana, netball, mpira wa wavu kwa wavulana na wasichana, mpira wa mikono, mpira wa kikapu kwa wavulana na wasichana, riadha kwa wavulana, wasichana na makundi maalumu pamoja na fani za ndani
Flaviana Bruno ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari ya wasichana Iringa ambaye pia amechaguliwa katika Timu ya Mkoa amesema yeye na wenzie wamejipanga kushiriki vyema katika michezo hiyo na kuhakikisha wanarudi na ushindi.
Nae Ayubu Salingwa Mwanafunzi mshiriki atakayekwenda katika mashindano hayo amemshukuru Mhe. Rita Kabati kwa kujitoa katika kuhamasisha wanafunzi hao katika kuona wanafanya maandalizi mazuri hadi kufikia siku ya mashindano na ametoa pongezi kwa Rais Samia kutoa nafasi ya uwepo wa michezo hiyo kwani inawajenga kiakili na kiafya n ani moja ya njia ya kufahamiana Zaidi hivyo akatoa ahadi yakwenda kufanya vizuri waendapo Mkoni Tabora
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa