“Nipende kuwaomba wataalamu wetu na watumishi wenzangu, ushirikano wa kutosha katika kuiletea maendeleo Manispaa yetu”
Hayo ameyasema Meya wa Manispaa ya Iringa leo Mh. Ibrahim Gwada katika kikao chake na wakuu wa idara na watumishi wote wa Manispaa makao makuu ya Halmashauri kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa
Sambamba na hilo Mh. Ngwada ametumia nafasi hiyo kujitambulisha rasmi mbele ya watumishi hao kwa nafasi yake na kutolea ufafanuzi juu ya mpango mikakati ambayo anaipatia kipaumbele katika uongozi wake hasa kwa kipindi cha kwanza mwaka 2021
Akiendelea kuzungumza mbele ya watumishi hao amesema, moja ya kipaumbele chake kwa mwaka huu ni kutoanzishwa kwa miradi mipya na hivyo kutumia muda mwingi kumalizia miradi yote iliyokwisha kuanzishwa hapo nyuma na vilevile kuboresha miradi ambayo ipo katika uchakavu ambapo ikikamilika itasaidia kuongeza kipato cha Halmashauri
Aidha amesema “nafikiri pia kuwa na vitu vya kushikika, kuundwa ambavyo vitaacha alama katika uongozi wetu hivyo tutaanza na kujenga jengo la TEMBO Bar, na sio lazima kutumia pesa zetu na mbadala wake tutatumia wadau na wabia katika ujenzi huo ambapo itatusaidia kuongeza kipato cha ndani” na akatoa wazo la kuboreshwa upya kwa ukumbi wa Halmashauri wa community centre katika ubora mzuri kama chanzo cha mapato
“katika elimu nimefikiri tuboreshe shule zetu ili ziwe katika muonekano mzuri ambao utasaidia wanafunzi wetu kupata elimu bora bila shida yoyote tukianza na madarasa, vyoo, maabara, mabweni, maktaba na vyote vinavyohitajika katkia shuke bila kusahau viwanja vya michezo” Mh. Meya aliongezea kwa kusema hayo huku akiahidi kuziwezesha timu za mpira wa miguu za ndani kufanya vizuri katika ligi
Mh. Ngwada pia amemaliza kwa kuwataka watumishi hao kutosita kumtafuta kwaajili ya ushauri, au changamoto zozote zinazo wakumba kwa mlengo wa kuzitatua na amewashukuru kwa ushirikiano waliouonesha kipindi cha uchaguzi kwa niaba ya uongozi wa Chama Cha Mapinduzi kumchagua Mbunge nanMadiwani wote kutokea chama hiko
"Msisite kunirekebisha na kuniambia mkiona siko sahihi, hii yote ni katika kujengana kwaajili ya maendeleo ya Halmashauri yetu na mnisaidie kufikia yale malengo ambayo tumejiwekea” Mh. Meya alisisitiza
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ndg. Hamid Njovu amemshukuru Mh. Mstahiki Meya kuzungumza na wataalamu huku akiwaasa watumishi kwa kusema “niwakumbushe wataalamu wenzangu kuwa kila zama ina kitabu chake, hivyo angalia nini inahitajika katika zama hizi na kuwajibika kama inavyotakiwa”
Ndg. Njovu anamaliza kwa kusema “Namshukuru sana Mh. Ngwada amenipunguzia matatizo makubwa sana yaliyokuwa changamoto katika Halmashauri yetu tena kwa kipindi hiki kifupi na kumuahidi kutoa ushirikiano wake kwake kwa kutekeleza mipango yao yote kwa asilimia zote kwa maendeleo ya Manispaa yetu"
“Kama mtamtumia vizuri Mh. Ngwada kwa kipindi hiki cha miaka 5 basi tutaleta maendeleo makubwa” Njovu akihitimisha kikao hicho ameyasema hayo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa