• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Miji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Environment and Cleaning
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Kazi
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma ya elimu
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya kilimo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya picha
    • Video za shughuli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba

VIKUNDI VINAVYONUFAIKA NA MIKOPO YA MANISPAA VYATAKIWA KUFANYA MAREJESHO KWA WAKATI

Posted on: June 29th, 2021

Timu ya Wataalam kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ikiongozwa na Kaimu Katibu Tawala  Bi. Saida Mgeni imefanya ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Miradi  ya maendeleo  inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa lengo la kuona mafanikio na changamoto katika Miradi hiyo

Vikundi viliyotembelewa ni pamoja na Envibright kikundi cha vijana kilichopo Gangilonga kinachjishughulisha na uoteshaji wa miti ya asili .Kikundi cha watu wenye ulemavu cha Amani group kilichopo Donbosco kinachojishughulisha na ufugaji wa Sungura na kikundi cha Tupendane vicoba kilichopo Frelimo kinachojishughulisha na ununuaji wa hisa pamoja na ufugaji wa kuku wa mayai

Bi.Mgeni   amewataka wanavikundi vinavyotekeleza miradi hiyo  kuwa  na umoja na  ushirikiano ili kuhakikisha  wanakuwa na mikakati ya kukuza uchumi wao

Myovela amesema kikundi cha Tupendane vicoba kinafanya  vizuri hivyo Mkurugenzi aone namna ya kutatua changamoto zao na kuwawezesha kupata eneo kubwa kwa ajili ya mradi wa ufugaji wa kuku  wa mayai ambao walianza kutekeleza tangu mwaka 2020  wakiwa na idadi ya vifaranga 200 na mpaka sasa wanafuga kuku zaidi ya 400

Aidha amevitaka vikundi vinavyonufaika na mikopo ya   Manispaa  katika  makundi ya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu kufanya marejesho kwa wakati ili kupata kiwango kikubwa zaidi pindi wanapomaliza mikopo hiyo na kuomba awamu nyingine pia kutoa nafasi kwa  wengine kunufaika na mikopo hiyo

'Rejesheni fedha kwa wakati ili na wengine waweze kunufaika na mikopo, fedha mlizopewa hazina riba mnaposuasua kurejesha mnawafanya wengine kukosa fursa hiyo muhimu alisisitiza Bi.Mgeni"

Benedict Dembe ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Muungano B. Ametoa wito kwa maafisa Maendeleo ya jamii kutoa elimu  ya ujasiriamali  kwa vikundi kwani itasaidia kuwapa uelewa wa matumizi sahihi ya fedha wanazopewa ili  waweze kutimiza malengo kusudiwa

Awali akisoma taarifa ya kikundi mbele ya Mgeni rasmi Bi.Redemta Mwinyi amemshukuru Mkurugenzi kwa kupitia ofisi ya Maendeleo ya jamii kwa kupata mkopo wa jumla ya shilingi milioni milioni 4 kwa awamu mbili ambazo zimewasaidia kukuza uchumi wa kikundi kupitia mradi huo wa ufugaji wa kuku. Na ameomba waweze kupewa fedha nyingine ili waweze kupanua eneo la ufugaji

Ziara hii ya siku tatu imeanza tarehe 29/6  hadi 1/7/2021 ambayo itatembelea miradi mbalimbali katika kata zote zilizopo Manispaa ya Iringa.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUONGEZWA MUDA WA KUCHUKUA FOMU YA UJENZI WA JENGO LA BIASHARA TEMBO BAR February 15, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA, 2023/2024 July 13, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI July 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 23, 2024
  • Soma zote

Habari za Hivi punde

  • PPP CENTRE YATOA MAFUNZO KWA WATAALAMU IRINGA MC

    April 04, 2025
  • ALUTE: "HAKIKISHENI MIRADI INAKAMILIKA KWA WAKATI NA KWA UBORA"

    December 21, 2024
  • UCHAGUZI HURU NA WA HAKI UNAHITAJI USHIRIKISHAJI - RC SERUKAMBA

    October 10, 2024
  • MSIGALA AWAONYA MAAFISA MAENDELEO KUJIHUSISHA NA MIKOPO HEWA

    October 05, 2024
  • Soma zote

Video

MEYA WA MANISPAA KUZIPIGANIA TIMU ZA MKOA KUPANDA DARAJA
More Videos

Viunganisho vya Haraka

  • National Examination Council of Tanzania
  • Watumishi Portal
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA,2023/2024
  • Sheria ndogo za Manispaa
  • Vivutio vya Utalii na Taarifda zake
  • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Tovuti Zinazofanana

  • Goverment Website
  • TAMISEMI
  • Iringa Region Website
  • IMtv Fahari ya Iringa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

Location Map

Wasiliana nasi

    Iringa Municipal Council

    Sanduku la Posta: 162

    Telephone: +255-2702647

    Mobile: 255-2702647

    Email: md@iringamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya usiri
    • Ukanusho
    • MMM
    • Ramani ya eneo
    • Huduma zetu

hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa