"Viongozi wa dini tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha kwamba tunatokomeza vitendo vya ukatili kupitia utoaji wa elimu katika nyumba za ibada na kupinga vikali tabia zinazopelekea matukio ya ukatili ndani ya jamii zetu"
Hayo yamezungumzwa na Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Iringa Bi. Tiniel Mbaga katika kikao kilichowahusisha viongozi wa dini mbalimbali kutokea kata 18 za Manispaa ya Iringa katika kutekeleza mpango wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia mpango mkakati wa mawasiliano,unaolenga kuchochea mabadiliko ya tabia zinazochangia matukio ya ukatili kufanyika.
Sambamba na hilo Bi. Mwantumu Dosi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii nae katika uwasilishaji wa mada yake amewaomba viongozi hao kusambaza jumbe mbalimbali zinazochochea mabadiliko dhidi ya tabia zinazopelekea kufanyika kwa vitendo vya ukatili
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa