Mh. Hapi ametoa agizo hilo katika kikao cha viongozi wote wa Dini waliopo Mkoa wa Iringa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ulipo Ofisi ya Mkoa ambapo alizungumza na viongozi wa dini na kuwaomba kufanya kazi kwa pamoja ili waweze kuijenga Iringa mpya.
Aidha amewataka Wakuu wa Wilaya wote katika Wilaya zao kuunda kamati za Amani zitakazo jumuisha Dini mbalimbali zinazowazunguka katika Wilaya zao ili kudumisha amani na kuleta wepesi katika utendaji wa kazi.
Amewashukuru viongozi wa Dini katika Mkoa wa Iringa kwa kuitikia wito na kuweza kuongea kwa pamoja na kuahidi kufanya kazi kwa karibu na viongozi hao wa dini ili kuhakikisha iringa inakuwa ya tofauti.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa