VYUMBA VIWILI VYA MADARASA NA OFISI ZA WALIMU ZAKABIDHIWA KWA MEYA WA MANISPAA YA IRINGA SHULE YA MSINGI KITWIRU.
Wafadhili kutoka kituo cha Amani Centre ndani ya Kata ya Kitwiru katika Manispaa ya Iringa, wamekabidhi madarasa mawili na ofisi za walimu kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mheshimiwa Alex Kimbe baada ya kusaidia umalizia wa vyumba hivyo vya madarasa.
Akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ofisi za walimu na vyoo vya walimu mkuu wa shule ya Kitwiru mwalimu Salome Sanga amesema ujenzi huo ulianza tarehe 18/5/2015 ambapo jumla ya shilingi milioni 46,650,100/= zimetumika katika ujenzi wa majengo hayo kwa mchanganuo ufuatao, Michango ya wanachi ni shilingi milioni,12,274,100/= wafadhili ambao ni AMANI CENTRE shilingi 10,500,000/=,serikali kutoka ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa shilingi 23,316,000/= na Ofisi ya Mbunge shilingi 560,000/=.
Akikabidhi majengo hayo Bwana Johan George kutoka Amani Centre amesema lengo lake na mke wake ni kuona watoto wanasoma katika mazingira mazuri hivyo haya yote yamefanyika kwaajili ya uwepo wa wanafunzi hawa katika Shule hivyo , wanafunzi ni watu muhimu katika maendeleo haya, aidha amewaasa walimu kufundisha kwa bidii kwani itakuwa haina maana kama mazingira ya kazi yatakuwa mazuri kwa majengo na madarasa alafu wanafunzi wakafeli. Hivyo amewaomba walimu kujitahidu kufanya kazi kwa bidii zaidi.
Akitoa shukrani baada ya kukabidhiwa majengo hayo Meya wa Manispaa ya Iringa Mheshimiwa Alex Kimbe amesea kuwa, ni jambo la faraja na kupendeza kuona ushirikiano uliopo kati ya Shule, Serikali na wafadhili umoja huu udumishwe na kuendelezwa kwa ustawi wa maendeleo ya wanafunzi na jamii ya watu wa Iringa.
Aidha mfadhili huyo ameahidi kujenga vyoo vya walimu katika shule hiyo ya Msingi Kitwiru.
Kwa habari zaidi tembelea tovuti ya Manispaa ya Iringa,
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa