Mkuu wa Wilaya ya Mbeya iliopo Mkoani Mbeya Dkt. Rashid Chuachua,amewapongeza waandishi wa habari wanawake kwa kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan,za kutangaza fursa za utalii na uwekezaji zilizopo nchini.
Dkt.Chuachua amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari wanawake waliojikita katika kuandika habari za utali na uwekezaji,kupitia kampeni yao ya kutembelea na kutangaza utalii na fursa za uwekezaji zilizopo nchini,wakati walipotembelea ofisini kwake wakiwa kwenye ziara yao ya siku tatu Mkoani humu ya kutangaza fursa hizo.
Aliwapongeza kwa namna wanavyo fanya ya kuangalia fursa za uwekezaji na kuhamasisha utalii katika maeneo mbalimbali nchini.
"Nawapongeza kwa sababu mnaunga mkono juhudi kikamilifu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye yeye ameamua kutangaza utalii kwa kufanya Royal Tour,kwa ajili ya kutangaza utalii na vivutio vya utalii,"
Sanjari na hayo amesema Wilaya hiyo na Mkoa kwa ujumla una fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali kiwemo kilimo na utalii.
Hivyo amewaomba wawekezaji kwenda kuwekeza katika Wilaya hiyo kwa ajili ya kuinua uchumi wa Mkoa,taifa na kutoa ajira kwa vijana.
Amesema suala la uwekezaji linalokwenda sambamba na uwekezaji katika sekta ya utalii,Wilaya ya Mbeya ina hali nzuri inayosaidia kustawi kwa mazao mbalimbali ambapo ina hali ya ubaridi na joto, hali inayofanya mazao mchanganyiko kuweza kustawi,
Naye mmoja wa wawekezaji mkoani humo,Mkurugenzi wa shule ya awali na msingi ya Paradise Mission,Ndele Mwaselela, alisema Mkoa huo una fursa na rasilimali nyingi,lakini changamoto iliopo ni kutovitangaza ili viweze kufahamika.
Mwaselela amesema,kupitia waandishi hao watasaidia kutangaza utalii na fursa za uwekezaji zilizopo mkoani humo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi,(CCM),Mkoa wa Mbeya Jacob Mwakasole,aliwapongeza waandishi hao kwa kuamua kutembelea Mkoa huo kwa ajili ya kutangaza fursa za utalii na uwekezaji.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa