"Nikiwa mmoja wa viongozi wa Halmashauri nawaahidi kuwasaidia mpate viwanja ambavyo mtalipia kwa awamu ikiwa ni kama motisha katika kutekeleza majukumu yenu ya kila siku"
Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe.Ibrahimu Ngwada alipokuwa anaongea na waandishi wa habari pamoja na wadau wa habari kwenye Maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani hapa Mkoani Iringa leo Mei 18. 2021 katika ukumbi wa Neema Craft
Mhe. Ngwada pia ametoa Rai kwa waandishi kujitokeza na kufanya shughuli mbalimbali zitakazowaletea mandelao, alisema "Msifanye kazi kwa kutegemea kipande kimoja cha mkate hivyo jaribuni kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazo wasaidia kuinua uchumi wenu"
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa Ndg. Frank Leonard katika hatuba yake amesema dhumuni la maadhimisho haya ni kuangalia na kulinda hali ya uwepo wa uhuru wa vyombo vya habari lakini kuwakumbuka waandishi wa habari waliopoteza maisha wakiwa katika majukumu yao ya kihabari pamoja na kukumbushana katika kutimiza majukumu yao ya kila siku kama wajibu wa Tasnia ya habari unavyowataka
Hata hivyo katika maelezo yake Ndg, Frank amesema pia, kwa mwaka 2020 Tanzania imekuwa nchi ya 124 kati 180 kwa uhuru wa vyombo vya habari kutokana na sababu ambazo ni kufungiwa kwa magazeti, kupigwa kwa waandishi, kutozwa faini zisizo stahiki, kufungwa kwa mitandao ya kijamii ya habari, kubadilishwa kwa kesi za jinai kuwa madai kwa uonevu
Aidha, ameeleza kuwa sababu nyingne inayopelekea kuanguka kwa tasnia ya habari ni baadhi ya makundi ya wanahabari kuingia katika propaganda za kuchafuana wenyewe kwa wenyewe bila sababu za msingi
"Tupendane, tushirikiane na kuishi kama ndugu tukishirikiana katika kukuza tasnia yetu." Mwenyekiti wa IPC Ndg, Frank akatoa wito kwa wanahabari waliohudhuria maadhimisho hayo
Maadhimisho hayo hufanyika kla mwaka Mwezi Mei na kwa mwaka huu 2021 yamefanyika leo na kuwashirikisha wanahabari na wadau mbalimbali wa Habari wakiwemo viongozi wa Serikali na wa vyama mbalimbali vya siasa,huku mada mbalibali zikijadiliwa ikiwemo Habari kwa Manufaa ya Umma.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa