Mhe. Ibrahim Ngwada, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa kuhakikisha wale wote wanaodaiwa madeni yanayotokana na mashine za ukusanyaji wa mapato POS kulipa madeni hayo mara moja.
Hayo ameyasema leo tarehe 29/9/2022 katika Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za hesabu za mwisho za Halmashauri ya Manispaa ya Iringa za kuishia tarehe 30 Juni 2022 ulilifanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Manispaa huku ukihudhuriwa na Mkuu Wilaya ya Iringa Mhe.Mohamed Moyo na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.
Mhe.Ngwada amesema ni lazima watu hao wapatikane na wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kurudisha fedha zote wanazodaiwa.
Aidha Ngwada amemuagiza Mkurugenzi na wataalam kushughulikia suala la wamachinga kwa kuhakikisha wanawapanga vizuri katika maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya kufanyia biashara zao.
Mhe.Ngwada amepongeza timu ya Menejimenti kupitia Sehemu ya Maendeleo ya Jamii kwa juhudi ya utoaji Mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani inayotolewa kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kwani katika kpindi cha Mwaka wa fedha 2021/2022 zaidi ya shilingi milioni mia saba (700) zimekwishatolewa katika makundi hayo.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kumazilizika kwa kikao hicho Diwani wa Kata ya Kwakilosa Mhe Hamid Mbata amesema Madiwani wamejipanga vyema kusimamia ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Manispaa na hawatakuwa na huruma kwa yoyote atakayeonekana kukwamisha utekelezaji huo .
Mhe Mbata amesema mkakati mwingine ni kuhakikisha wanaibua vyanzo vipya vya mapato na kuboresha vile vya zamani kwa lengo la kuongeza mapato ya Halmashauri ili kuwaletea wanachi maendeleo.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO MANISPAA YA IRINGA.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa