Kaimu wa Mkuu wa Mkoa wa İringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Peres Magiri amewataka wafanyakazi Mkoani humo kuhakikisha wanapinga vikali ukatili wa kijinsi kwa Wanawake na Watoto na kutokomeza tatizo la Udumavu ili kupata nguvu kazi bora ya Maendeleo
Peres ameyasema have leo tarehe 1/5/2023
wakati wa sherehe ya Wafanyakazi (Mei Mosi) iliyofanyika kimkoa katika Halmashauri ya Mji Mafinga katika viwanja vya Mashujaa.
Aidha Mhe. Magiri amesema kuwa ni wakati sasa wa wafanyakazi kusimama kuwajibika na kupambana kwa kufanya kazi kwa bidii huku wakihakikisha wanazitatua Changamoto mbalimbali zinazo kwamisha Maendeleo ya Taifa ikiwa ni pamoja na suala la ukatili na udumavu kwa watoto.
Mhe. Magiri pia amewataka wanafanyakazi wote kufanya maandalizi mapema ya kuweka akiba itakayowasaidia pindi wanapoelekea kustaafu.
Akitoa taarifa kwa Niaba ya Wafanyakazi wote Mratibu wa TUCTA Mkoani İringa ndugu Kuguru Kitambuka ameiomba Serikali kupunguza kodi ya wafanyakazi pia kukiangalia Kikokotoo
Sambamba na haya pia Mhe. Peres Magiri amewakabidhi zawadi mbalimbali kwa wanafunzi bora waliokuwa wafanyakazi bora.
Imetolewa na kaimu Mkuu wa kitengo cha MawasilianoiSerikalini Manispaaya ya Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa