WAHITIMU WAJESHI LA AKIBA WATAKIWA KUWA MFANO KWA JAMII
Mkuu wa wilaya Iringa Mh. Richard Kasesera amewataka Mgambo wote wa Jeshi la Akiba kuzingatia maadili na nidhamu ya kazi ili kuimarisha ulinzi na usalama wa Manispaa ya iringa na Mkoa kwa ujumla.
Mh,Kasesera ametoa wito huo katika Hafla fupi ya kuhitimisha mafunzo ya jeshi la akiba yaliyofanyika Shule ya Msingi Mlandege ambapo mbali na kuhitimisha mafunzo hayo ameteuwa wahitimu 9 kujiunga na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) kwa mwaka 2017.
Mbali na hayo ameuangiza Uongozi wa Manispaa ya Iringa pamoja Na Makampuni ya ulinzi kutoa ajira kwa Mgambo waliopitia mafunzo ya Jeshi la akiba na kusisitiza walipwe Mishahara isiyopungua kima cha chini cha Kiserikali.
Aidha amewataka kushirikiana na Jamii na kuwa walinzi wa mfano kwa kuwasaidia Wananchi matatizo mbalimbali ya kiusalama zaidi pia wawe wanatoa taarifa za Rushwa bila kusita endapo watabaini kuna vitendo au viashiria.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa