Wakuu wa Idara na vitengo wa Halmashauri ya Manispaa wametakiwa kubuni na kutafuta njia ya kuweza kuchoche mapato ya Manispaa ili kuweza kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya Ndugu Hashim Komba alipokuwa akizungumza na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa katika ukumbi wa Manispaa.
Amesema wakuu wa Idara wanatakiwa waone ufahari kumshauri mkurugenzi wa Manispaa kuhusu kukusanya mapato na kila Idara ipange kubuni vianzia vipya na jinsi gani itaweza kushauri katika ukusanyaji wa mapato.
Ndugu Komba awewataka wakuu wa Idara na vitengo kuwa wazalendo katika kutimiza wajibu wao wa kazi kwani kwa kufanya hivyo watatoa huduma nzuri kwa wananchi na walio chini yao hasa kwa kuzingatia mwenendo wa serikali.
“Lazima watumishi tutawaliwe na uzalendo kwa kutumia taaluma zetu,weledi wetu na ubunifu katika kutimiza wajibu wetu”. Amesema Komba.
Amesema uzalendo ni pamoja na kutumia taaluma katika kuwahudumia wananchi hivyo kila Idara iwajibike kusogeza huduma kwa wananchi kwa kuwafuata maali waliko.
Aidha amewataka kujenga utamaduni wa kuwasikiliza watumishi walio chini yao hadi ngazi ya kata ili kupunguza malalamiko na kufanya kazi kwa ushirikiano na ufanisi mkubwa kwa kufanya hivyo wananchi watapokea huduma nzuri.
Pia amezitaka Idara zinazofanya kazi kwa ukaribu na wananchi hasa Idara ya Mipango miji, Maendeleo ya Jamii, Utumishi na Idara ya fedha kutoa majibu fasaha kwa wananchi na kuweka muda sahihi wa kujibu kero za wananchi. Hii itasaidia kupunguza upotevu wa nyaraka za serikali na huduma kutolewa kwa ufanisi.
Ameongeza kuwa lugha mbaya kwa wananchi, chuki, upotevu wa nyaraka za serikali na ucheleweshaji wa huduma kwa wanachi ndio kunapelekea wananchi kujenga chuki kwa serikali yao. Hivyo amewataka watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia uzalendo kanuni na sheria za kazi.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa