Mkuu wa wilaya ya Iringa ndugu Richard kasesela ametoa maagizo kwa Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2020 wanapata nafasi .
Kasesela ameyasema hayo leo 8/12/2020 katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa alipokutana na watendaji hao wa Manispaa kujadili mustakabali wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 202I.
Kasesela ametoa maelekezo hayo kwa wakuu Idara na vitengo kuacha kwenda likizo ya krismass na mwaka mpya 2021 badala yake wajiwekee mikakati madhubuti ya kumalizia ujenzi wa vyumba vya madarasa ilikuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika Halimashauri hii wanapata nafasi ya kusoma bila kupata changamoto zo zote.
Kwa mujibu wa kaimu Afisa Elimu Manispaa Bi Elitruda Mtewele amesema jumla ya wanafunzi 1323
waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza hawajapata nafasi ambapo vyumba vya madarasa 27, meza pamoja na viti1590 vinahitajika kwa ajili ya wananunzi hao kujiunga na kidato cha kwanza.
Aidha Mtewela amesema mikakati ya kukakilisha majengo ya madarasa pamoja na madawati imekwishafanyika na wako katika hatua za mwisho za ukamilishaji zoezi hilo.
Nae Mkurugenzi wa Maniapaa ya Iringa Hamid Njovu amemuhakikishia Mkuu wa wilaya kuwa yuko tayari kutekeleza majukumu hayo pamoja na timu hiyo ya menejimenti kwa haraka na ifikapo Januari 2021, shughuli hizo zitakamilika na wanafunzi watasoma bila tatizo lolote.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa