Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ndugu Ally Happi amewataka wakuu wa Idara na vitengo kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuwapa elimu ya ujasiriamali kama,kilimo na ufugaji bora wenye tija ili waweze kujikwamua kiuchumi. Kwani kwa kufanya hivyo watajitegemea na kupunguza wimbi la wananchi ambao ni tegemezi.
Kauli hiyo ameitoa leo 19/12/2020, katika ukumbi wa chuo cha afya alipokuwa akizungumza na viongozi mbali mbali wa chama na Serikali Mkoa wakiwemo waheshimiwa Wabunge wenyeviti wa Halmashauri pamoja na wakuu wa Idara na vitengo kutokal Halimashauri za wilaya,na Mkoa.
Aidha Happi amesema lengo la kikao hicho ni kuweka mikakati ya kutekeleza Ilani ya CCM ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 -2025.na maelekezo ya Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Magufuli wakati wa kufungua bunge la 12 tarehe 13 Novemba 2020.
Katika kikao hicho mada mbalimbali zilitolewa ikiwemo,mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya uchaguzi mkuu 2015, Masuala ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi,Nafasi ya serikali za mitaa katika kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi
Akichangia mada katika kikao hicho Mbunge wa Iringa Mjini mhe. Jesca Msambatavangu amesema ipo haja ya kuwatumia Maafisa Tehama kuhakikisha wanatoa elimu ipasavyo kwa jamii na kutangaza vivutio vilivyopo katika Mkoa wetu pamoja na shughuli mbalimbali za kilimo,ufugaji na ujasiriamali.
Akichangia mada katka kikao hicho Mkuu wa wilaya ya kilolo Bi.Asia Abdallah amesema wananchi wanahitaji Elimu na uhamasishaji katika suala la ujasiriamali ili waweze kujikwamua kiuchumi na kupunguza tatizo la ajira.
Akifunga kikao hicho Happi amewataka wakuu wa idara na vitengo waanzishe kambi kwa wanafunzi wenye madarasa ya mitihani ya kidato cha pili cha nne na cha sita kwenye shule za sekondari ili kuhakikisha wanafunzi wanafaulu vizuri katika masomo yao,.pia ameagiza kila Halmashauri iwe na karakana kwa ajili ya matengenezo ya meza, viti vya shule na vya Halmashauri vinapoharibika.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa