Rai imetolewa kwa jamii kuhakikisha wanawatoa nje watu wenye ulemavu ili waweze kuhesabiwa katika Sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 2022 mwaka huu.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Queen Sendig katika kongamano na Bonanza la michezo kwa watu wenye ulemavu lililofanyika Julai 9 2022 katika uwanja wa Bustani ya Manispaa ya Iringa.
Aidha Mhe.Sendiga amesema Sensa ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii hivyo watu wenye ulemavu nao wanahaki ya kuhesabiwa kwa kufanya hivyo Nchi yetu itaweza kupanga mipango ya Maendeleo kupitia takwimu hizo.
Mhe.Sendiga amempongeza Mbunge wa viti maalum na Mratibu wa kongamano hilo Mhe.Ritta kabatii ambaye pia ni mwanzilishi wa mfuko wa Rita kabati kwa kuyajali makundi maalum na kuhamasisha jamii kumuunga mkono.
Ndugu Raymond Nyenza ni Mratibu wa Sensa Manispaa ya Iringa amesema umuhimu wa takwimu zitokanazo na Sensa ni takwimu hizo zitaonyesha uwiano kati ya watoto waliofikia umri wa kwenda shule na wale ambao hawajafikia umri huo,pia kupanga huduma za afya ya mama na mtot,,huduma za Afya Elimu na kuboresha mazingira ya kazi.
Mhe.Ritta kabati Mbunge wa viti Maalum na Mratibu wa kongamano hilo amesema lengo la tukio hilo ni kutoa elimu ya sensa na kuhamasisha jamii ushiriki wa makundi maalum kuhesabiwa.
Naye Mjumbe wa kamati kuu (CCM) Bi.Theresia Mtewele amesema Serikali imeongeza bajeti ya kuhudumia kundi maalum kwa kujua idadi yao.
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mhe..Jesca Msambatavangu amepongeza juhudi zinazofanywa na mhe.Ritta kabati kuwahudumia watu wenye ulemavu katika mahitaji yao muhimu na kusema yuko pamoja katika kuhakikisha kundi hilo haliachwi nyuma.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali Mhe.Samia Suluhu Hassan alituma ujumbe kwa wananchi na kuwahakikishia kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko pamoja nao.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa