Wafanya biashara wadogo wadogo halimaarufu kama Machinga waliopo Manispaa ya Iringa wameishukuru Serikali ya awamu yatano inayoongozwa na Docta John Pombe Magufuli kwa kuwajali na kutambua uwepo wao kama wamachinga hususani maeneo ya Mjini.
Shukrani hizo za dhati zimetolewa na Mwenyekiti wa wamachinga pamoja na katibu wao kwenye kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela chenye lengo lakukutana na wamachinga wote pamoja na viongozi wao ili kuweza kuzisikiliza changamoto zinazowakabiri na kuzitatua ikibidi kwa kufuata sheria na kanuni kama tamko la mweshimiwa Rais linavowataka.
Aidha bwana Zeche Zabron Mwenyekiti wa Machinga Iringa Mjini amesema licha ya kuwepo bado na changamoto mbalimbali zinazowakabiri kama kuvamiwa na migambo na kumwaga bidha zao maeneo ya Mjini bado wanamshukuru Mh. Rais Magufuli kwa kutoa agizo la kuwaacha na kuwatengea maeneo rafiki ya kufanya biashara zao Mijini ikiwa nipamoja na kurasimisha biashara hizo kiuwalali na sio kuwafukuza kama mwanzo huku wakiahidi kuiunga mkono Serikali ya awamu ya tano kwa asilimia zote za kimaendeleo hasa kwa machinga ili kufikia Uchumi wa kati kiviwanda ifikapo 2020.
Mwisho Mkuu wa Wilaya Mh. Kasesela amehitimisha kwa kuwataka wamachinga wote kuwa na vitambulisho vitakavyowatambulisha kisheria na eneo husika wanalofanyia kazi, pia amewasisitiza wajiunge na mifuko ya kijamii kama Bima ya afya na ya mafao ya uzeeni ili kuwasaidia kutoka kwenye wimbi la umasikini pamoja nakuweza kupata mkopo kutoka mashirika na taasisi za kifedha
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa