Wamiliki wa nyumba za wageni pamoja na Hotel ndani ya Manispaa ya Iringa wameaswa kuzingatia ulipaji wa kodi kwa uaminifu pamoja na uboreshaji wa huduma wanazotoa katika maeneo yao.
"Mimi naamini endapo mkiwa waaminifu kulipa kodi kwa wakati na kuwa sahihi basi hakutakuwa na shida za kusumbuana katika maeneo yenu ya biashara"
Hayo yamezungumzwa leo tarehe 22/12/2020 na Saad Ishabailu Mwenyekiti wa kamati ya ukusanyaji mapato Manispaa ya Iringa katika kikao kilichowakutanisha wamiliki wa nyumba za wageni na hoteli pamoja na kamati ya ukusanyaji mapato katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa
Aidha kikao hicho kimefanyika kikiwa na agenda kubwa ya kujadili masuala ya usimamizi, uendeshaji wa nyumba za kulala wageni na ulipaji wa kodi mbalimbali kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Pia katika mazungumzo yake Ndugu.Ishabailu amewataka wadau hao kuboresha mazingira katika biashara zao kwani kwa kufanya hivyo wateja wao watafurahia huduma zao hasa kuwa na mazingira bora na safi
Sambamba na hayo, wamimiki hao wametoa ombi kwa Serikali kuwapunguzia mlundikano wa kodi ambazo wanazitoa na kuzifanya kuwa katika mlengo mmoja. Alisema ndugu Cosmass Msigwa mmoja wa wamilimi wa Nyumba ya wageni walioshiriki kikao hicho
Nae Mjumbe wa kamati ya ukusanyaji wa mapato Manispaa ya Iringa, ndugu Noel Shilembi aliwataka wadau ambao hawajakata leseni za biashara, kuhakikisha wanafanya hivyo ili kuepusha usumbufu usio wa lazima
Kamati hiyo ya ukusanyaji mapato ilipata fursa ya kusikiliza na kupokea changamoto mbalimbali za wafanyabiashara huku ikiahidi kuzifanyia kazi mara moja.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa