Wanafunzi 11 na Mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Uyole, iliyopo katika Halmashauri ya Manispaaya Iringa wamelazwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoani humo baada ya kupigwa na radiwakati wakiendelea na masomo.
Tukiohilo limetokea asubuhi ya Jumatatu ambapo mvua ilikuwa inanyesha na wanafunzihao wa darasa la saba wakiwa darasani.
Mkuuwa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amefika hospitalini hapo kuwajulia haliwaathirika hao na kueleza kuwa Serikali imefanya jitihada za kuwahudumiawahanga kwa uharaka baada ya kupokea taarifa ya kutokea kwa tukio hilo nakusema hali zao zinaendelea vizuri.
MstahikiMeya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada amewasihiwananchi kutohusisha tukio hili na imani za kishirikina na waamini ni tukiolinaloweza kutoka muda wowote na sehemu yoyote hivyo wasihusishe na vituvingine.
“Nichukuefursa hii kutoa wito kwa wananchi ambao wamepeleka watoto wao katika shule hiiwasiwe na hofu na watambue hili ni tukio la kawaida kama matukio mengine naninaomba msihusishe tukio hili na imani za kishirikina kwani inaweza kutokeasehemu yoyote, natamka haya kwasababu nasikia kuna baadhi ya wananchi wanahusishana imani za kishirikina, kitu ambacho hakipo” Amesema Ngwada
MstahikiMeya aliongeza kwa kusema amepokea na kuufanyia kazi ushauri uliotolewa nawananchi juu ya kufanyika kwa Dua/Maombi katika shule hiyo ili kuondoa mikosi.
Mkuuwa Idara ya Magonjwa ya Dharula wa Hospitali ya Rufaa Mkoani Iringa Dkt. HurumaMwasipu amethibitisha kupokea wahanga wa tukio hilo na kusema kuwa walifikishwawakiwa na majeraha madogo madogo na kupatiwa matibabu huku wengine wakitarajiwakuruhusiwa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa