Timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya katibu Tawala Mkoa imetembelea na kukagua Miradi ya shule za Sekondari zilizopo Manispaa ya Iringa kwa lengo la kuona maendeleo yake ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu kassim Majaliwa kuwa kila Halmashauri ihakikishe wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanapata madarasa ya kutosha kusomea
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa katika ziara hiyo ni Shule ya Sekondari ya Nduli, Shule ya Sekondari Kihesa, Shule ya Sekondari Mtwivila(umoja), Shule ya Sekondari Mlamke,Shule ya Sekondari Mkwawa, Shule ya Sekondari Isakalilo, Shule ya Sekondari Mlandege, Shule ya Sekondari Igumbilo na Sekondari ya Ipogolo
Akitoa taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa, Kaimu Afisa Elimu Sekondari Elitruda Mtewele amesema jumla ya wanafuzi 3613 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza Manispaa ya Iringa ambapo ana uhakika wanafunzi wote watapata nafasi ya kuendelea na masomo kutokana na jitihada za umaliziaji ujenzi wa madarasa zinazofanywa na uongozi wa Halmashauri
Naye Mkurugenzi Manispaa ya Iringa Hamid Njovu ameishukuru timu hiyo ya wataalamu kutembelea miradi hiyo kwani imekuwa chachu ya kuongeza jitihada za umaliziaji ujenzi kwa wakati na ameahidi kusimamia vyema ujenzi huo kuwa ifikapo januari 11 wanafunzi wote waliochaguliwa wataingia madarasani bila wasiwasi wo wote
Naye Katibu Tawala msaidizi Uchumi na Uwezeshaji ndugu Elias Luvanda amesema uongozi wa Mkoa unathamini kazi za ujenzi wa miradii inayoendelea kutekelezwa Manispaa na ameshauri Halmashauri kuwa na mipango mikakati ya utekelezaji miradi hiyo pia iongeze usimamizi kwa fedha wanazopeleka katika miradi hiyo na waongeze idadi ya mafundi ili kuongeza kasi ya ujenzi ili kumaliza kwa wakati Pia ameitaka Halmashauri kupima maeneo ya shule ili maeneo hayo yawe na hati miliki
Ziara hiyo ilifanyika tarehe 22/12 mwaka huu na kuhudhuriwa na timu ya Menejimenti ya Manispaa ya Iringa ikiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa