Wananchi wa Kata ya Nduli, Mtaa wa Kupululu Manispaa ya Iringa wamempongeza Diwani wa kata hiyo Mhe. Bashiri Mtove kwa jitihada anazofanya kusaidia ujenzi wa Shule mpya ya Msingi ambayo itapunguza changamoto katika Sekta ya Elimu kwenye Kata hiyo
Mhe. Mtove akizungumza na wananchi hao wakati akikabidhi mifuko 30 ya saruji leo tarehe 2.06.2021 kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mhe. Jesca Msambatavangu, amesema anatamani kuona wanashirikiana vyema na wananchi katika kukamilisha ujenzi huo ambao utaleta manufaa katika jamii
Aidha Mhe. Mtove amewashukuru wananchi kwa kujitoa kwaajili ya ujenzi huo mpaka hapo ulipofikia na kuwaahidi kuwa ataendelea kuwashirikisha wadau wengine watakaosaidia kuongeza nguvu ya umaliziaji wa jengo hilo
Baton Zakaria Nzalarila ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Kipululu, ametoa shukrani kwa niaba ya wananchi kwa Mhe. Mbunge na Diwani wao kwa kujitoa katika ujenzi huo huku akiwaomba wadau wengine kujitokeza kuwasaidia kuongeza nguvu ili kufikia malengo waliyokusudia
"Tunaamini mradi huu utakapokamilika utatatua changamoto zilizopo katika Sekta ya Elimu na kufanya wanafunzi kupata Elimu kwa urahisi kwani kwasasa hutembea umbali mrefu kwenda shuleni" alisema Witness Kiwele, mmoja wa wakazi katika mtaa wa kipululu
Bi. Faustina Mdete ambaye ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kipululu ameeleza kuwa moja ya tatizo la watoto wao kushindwa kufanya vizuri kitaaluma ni umbali wa shule ambazo wanasoma hivyo ameiomba Serikali kuwasaidia kwa haraka ili kuepukana na changamoto hiyo
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa