I
“Nawagiza wananchi wote kuwa walinzi na kulinda alama za barabarani na sio kuzin’goa na kuuza kama chuma chakavu.” Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli katika hafla fupi ya kuzindua barabara ya Iringa Migori Fufu yenye urefu wa kilometa 189 iliyofanyika katika kijiji cha Ndolela mkoa wa Iring
Dkt Magufuli amewataka wananchi kutumia fursa ya Barabara hiyo kuwekeza katika kilimo kwani ni njia ya haraka ya kusafirisha mazao mbalimbali kutoka mashambani kulelekea sehemu mbali mbali za masoko zilizopo ndani na nje ya nchi
Aidha amewapongeza wadau mbalimbali waliosaidia ujenzi wa barabara hiyo ikiwemo Banki ya maendeleo ya Africa (ADB) pamoja na ubalozi wa Japan Tanzania (JAICA) Kwa kutoa mkipo bila masharti (soft loan) na kuwataka kuendeleza ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania pamoja Taasisi hizo.
Pia amewapongeza wanachi wa Iringa kwa kujitokeza kwa wingi na kusisitiza kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kusadia wananchi wote wenye kipato cha chini kwa kuwekeza katika miundombinu mbalimbali kama vile barabara,umeme, reli, pamoja na kuweka mazingira rafiki ya Viwanda ili kufikia uchumi wa kati.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa