Wananchi wa Kata ya Kihesa, Manispaa ya Iringa wameaswa kuzingatia usawa wa baba na mama katika malezi ya watoto na kukemea suala la unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto
Hayo yameelezwa na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Manispaa ya Iringa siku ya jana mei 29, 2021 katika mkutano wa hadhara uliohusu kampeni ya ushirikishwaji wa wanaume katika suala la malezi pamoja na kupinga unyanyasaji wa kijinsia na ukatili kwa watoto
Akizungumza katika hadhara hiyo Bi. Josephine Mwaipopo ambaye ni Afisa Ustawi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa amesema watoto na wanawake ni makundi yanayoathirika zaidi kutokana na ukatili wa kijinsia hali inayopelekea kupungua kwa nguvu kazi katika uzalishaji hivyo, kuitaka jamii hiyo kuepukana na matendo ya namna hiyo
Sambamba na hilo Bi.Josphine amewataka wazazi kuimarisha ulinzi wa watoto wao dhidi ya matukio ya ubakaji na ulawiti ambayo kwa sasa yameonekana kuripotiwa sana katika ofisi za ustawi na vituo vya polisi
William Rashid Mkazi wa semtema A amesema utandawazi unasabibisha kutokea kwa ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto wa kike kwasababu hutumia nafasi ile kuyaiga mambo yasiyo na maadili na kuyafanya katika jamii kiuhalisia hali inayosababisha kutokukoma kwa matendo ya ubakaji na ulawiti
Aisha Mabruk ni mkazi wa Semtema amesema ukosefu wa hofu ya Mungu kwa jamii nzima pamoja na imani za kishirikina zinachangia kufanyika kwa matendo ya ukatikili wa kijinsia, ubakaji na ulawiti kwa mtazamo wa kudhani ndio mafanikio kuitaka jamii kuacha tabia hiyo mara moja
David Swebe, Mtendaji wa Kata ya Kihesa amewashukuru waratibu wa mkutano huo uliofanyika katika eneo la uwanja wa Semtema B kwa utowaji wa elimu dhidi ya kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia na amewataka wanachi kuzingatia maadhimio mbalimbali waliyokubaliana katika kutokomeza vitendo hivyo ikiwemo kutoa taarifa mara moja zenye kuashiria au kutokea kwa vitendo hivyo na sio kuyamaliza wenyewe, kutoa elimu kwa kila kaya, kuimarisha ulinzi na malezi bora ya wazazi wawili kwa watoto wao na jamii kwa ujumla.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa