Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Jamhuri William, amewataka wanaume Mkoa wa Iringa kuwa mstari wa mbele katika upimaji wa maambukizi ya VVU Kupitia kampeni ya upimaji iliyozinduliwa rasmi mkoa wa iringa.
Aidha Mh. Jamhuri amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuhamasisha wananchi mkoa wa Iringa kujitokeza kupima ili kujua afya zao na kuwa mstari wa mbele kujitokeza kupima kila wakati.
Maadhimisho haya yamefanyika katika uwanja wa Mwembetogwa na kuhudhuriwa na viongozi kutoka katika taasisi binafsi, za kidini, na za kiserikali ndani ya mkoa wa Iringa , vyombo vya usalama pamoja na wananchi
Maadhimisho hayo yameongozwa na kauli mbiu isemayo “FURAHA YANGU PIMA JITAMBUE ISHI” lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kuwa na utamaduni wa kupima afya zao kila wakati.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa