MGOMBEA Ubunge katika jimbo la Iringa mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Jesca Msambatavangu amewataka wanachama wa chama hicho kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha wanalinyakua jimbo hilo.
Ametoa kauli hiyo wakati wa hafla maalum ya mapokezi yake, yaliyoandaliwa kwa ajili ya kumtambulisha rasmi kwa wanachama wa CCM pamoja na kutafuta wadhamini, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Chama hicho, uliopo eneo la Sabasaba mjini hapa.
Aidha Msambatavangu amewataka wapinzani kujiandaa kisaikolojia, kwani watashughulikiwa kikamilifu katika sanduku la kura, huku akijigamba kuwa watafanya hivyo kupitia kwa umoja wa wanawake wa CCM (UWT) pekee, kabla ya wanachama wa jumuiya nyingine.
Ndugu Msambatavangu alipata fursa ya kuzunguka na kutambulishwa kwa wananchi wa maeneo ya Kihesa kilolo, Mashinetatu na Samora ambapo wananchi wengi walionekana kufurahishwa na mgombea huyo, huku wakieleza kuwa ndiye jibu la kero zao.
Awali Mwenyekiti CCM wilaya ya Iringa mjini, Ndugu Said Rubeya amesema kwa muda mrefu chama hicho kimekuwa kikihitaji mgombea atakayeshughulika na shida za watu; na amesema
Ndugu Jesca ni mtu sahihi kwani ni chaguo la watu. Hata hivyo Mwenyekiti huyo, amewaomba wanachama wote wa CCM kuunganisha nguvu zao ili kuhakikisha kuwa wanalirudisha jimbo hilo, lililokuwa chini ya chama cha upinzani, katika usimamizi wa chama chao.
Mapokezi ya mgombea huyo yamepambwa na maandamano makubwa yaliyohusisha wanachama, bajaji, bodaboda na magari huku kivutio kikubwa kikiwa gari kubwa maalum litakalotumika wakati wa kampeni za CCM mkoani hapa mwaka huu.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa