“Fedha mlizozipata mzitumie kwaajili ya biashara na malengo kusudiwa na si vinginevyo ili wakati wa kufanya marejesho msiyumbe kurejesha fedha hizo”Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela alipokuwa akifungua sherehe za utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana kutoka katika kata 18 zilizo katika Manispaa ya Iringa wenye thamani ya shilingi milioni 140.
Amesema mikopo inayotolewa inatakiwa kurejeshwa kwa wakati ili wananchi wote wa Manispaa ya Iringa waweze kunufaika na mikopo hiyo. Aidha amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii na Ofisi ya Mkurugenzi kuendelea kutoa elimu ya ujasiliamali kwa wananchi kwani kwa kufanya hivyo mikopo inayotolewa itatumika kwa malengo kusudiwa.
Akikabidhi hudi kwa vikundi 42, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mheshimiwa Alex Kimbe amesema fedha zilizotolewa zimetoka katika makusanyo ya ndani ya Manispaa, hivyo wananchi wote kwa awamu wanatakiwa kufaidika na mkopo huo ambao unatolewa kwa marejesho ya mwaka mmoja. Ameongeza kuwa katika sherehe za mbio za mwenge mwaka huu mwezi wa tano vipo vikundi vingine ambavyo vitapata mkopo kutoka Manispaa hivyo wananchi wajitokeze kupitia kata zao weweze kuonana na maafisa maendeleo ya Jamii ili kupata taratibu za mikopo hiyo.
Sherehe ya kukabidhi hudi kwa vikundi imefanyika katika ukumbi wa hallfaer uliopo katika Kata ya Kitanzini Manispaa ya Iringa na kuongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Mkuu wa Wilaya, Madiwani, Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na wataalamu mbalimbali.
Aidha katika kipindi cha mwaka 2017/2018 Manispaa ya Iringa imetenga kiasi cha shilingi 418,082,700/= ambayo ni asilimia 10 ya mapato ya ndani kwaajili ya mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake ambapo mpaka sasa Manispaa imeshatoa mikopo nyenye thamani ya shilingi milioni 250 sawa na asilimia 60.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa