Wanawake wametakiwa kupambana na changamoto wanazokumbana nazo katika familia na jamii na kuacha visingizio vinavyopelekea kuwakwamisha mafanikio yao.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Queen Sendiga alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo Mkoa wa Iringa yamefanyika katika viwanja vya Mwembetogwa.
Sendiga amesema kuwa wanawake licha ya kupambana ili kukabiliana na changamoto za maisha bado mfumo dume umekuwa changamoto kubwa ya kuwakwamisha kufikia malengo.
Mhe.Sendiga amewataka wanawake kuwa wa Kwanza kutetea Haki zao na kuhakikisha jambo walilokusudia kulifanya linatimia.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa Mkoa wa Iringa wanawake wanajitaidi Sana juu ya masuala ya ujasiriiamali lakini bado haujawa mkubwa ili kufikia ujasiliamali wa kimataifa.
Awali Mbunge wa Iringa mjini mhe Jesca Msambatavangu amewataka wanawake kujiona ni wa thamani na kujiamini kwa kile wanachokifanya.
Naye Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Moyo amewataka wanawake kuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii juu ya zoezi la sensa ya watu na makazi ili kukamilisha zoezi hilo kwa maendeleo ya Taifa letu.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na mamia ya wanawake kutoka wilaya zote za Mkoa wa Iringa wakiwemo viongozi mbali mbali wa chama na Serikali yamebeba kauli mbiu ya kizazi cha haki na usawa tujitokeze kupiga kura.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa