Na Mwandishi Wetu, Iringa
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amekabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi bilioni 1,143 ,749,140 iliyotolewa kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu Mkoani Iringa.
Mhe.Ummy amekabidhi hundi hiyo leo Novemba 23, 2021 kwenye kongamano la uwezeshwaji wanawake kiuchumi na kijamii tukio ambalo lilishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali na kufanyika ukumbi wa Kichangani Manispaa ya Iringa.
Alisema ni jukumu la kila Halmashauri ya wilaya na Mji kuhakikisha zinatenga asilimia kumi ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
"Sitamuonea aibu Mkurugenzi yeyote ambaye hatatenga na kutoa fedha kwa wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu," alisema Mhe.Ummy.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe.Queen Sendiga alisema lengo la kongamano hilo ni kuwaunga mkono kinamama wajasiriamali, kujadili fursa za kijamii, kupeana uzoefu na kujifunza kwa waliofanikiwa na namna ya kutatua changamoto zinazojitokeza.
Naye Mbuge wa jimbo la Iringa mjini, Mhe Jesca Msambatavangu, aliwaasa kina mama kuwalea watoto wao vizuri kwani kwa kufanya hivyo itapuguza matukio ya ubakaji na ulawiti .
Katika kongamano hilo mada mbalimbali zilitolewa pamoja na ulinzi na usalama kwa mtoto, Uchumi,Afya ya akili,Saikolojia na lishe.
Jumla ya vikundi 131 vimenufaika na mkopo wa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wametoa sh milioni 92,000,000 kwenye vikundi 23 kwa kipindi cha Julai-Septemba,
Halmashauri ya wilaya ya Iringa wametoa sh m 272.,000,000 kwa vikundi 33 huku kilolo wakitoa sh m 204,000,000 ambazo zimetolewa kwa vikundi 15
Mafinga imetoa shilingi m 249,169,140 kwa vikundi 11 na Mufindi wametoa jumla ya sh m.326,580,000 kwa vikundi 19.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa