WANAWAKE WAPEWA ELIMU
kuelekea Maadhimisho ya siku ya Mwanamke Duniani, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imefanya kongomano la WANAWAKE tarehe 5-03-2024 katika ukumbi wa shule ya Sekonari Lugalo ambapo wataalamu wametoa elimu ya Bashara, lishe na ujasiriamali wanawake na Uongozi ambapo wanawake wamejitokeza kwa wingi katika Kongamano hilo.
Afisa Maendeleo ya jamii wa Manispaa, Ndg. Paul Mpwehwe amesema lengo la kuaandaaa kongomano hilo ni kuona jinsi gani wanawake wanazigeuza changamoto kuwa fursa .
Aidha Mpwehe amewataka washiriki kusikiliza kwa umakini mafunzo hayo ambayo wataalamu mbalimbali wametoa elimu ili kumuinua na kumjenga mwanamke katika jamii anayoishi.
Mhe. Dora Nziku ni muwakilishi wa Mwenyekiti waKamati ya Sherehe hiyo ya wanawake Manispaa amewasihi akina mama waweze kujitokeza kwa wingi katika mambo ya uongozi pasipo kuwa na uoga wowote na kuwa wanawake wasikubali kubaki nyuma kama zamani.
"WANAWAKE wenzangu hiki ni kipindi Cha chaguzi mbalimbali hivyo jitokezeni mkagombee nafasi za uongozi kwenye maeneo yenu, tujiamini kwani tunaweza saana."
Nziku amesema maneno hayo alipokua akifunga kongamano hilo la WANAWAKE ambalo lilifana kwa kuwa wanawake walipata kujifunza masuala mbali mbali ikiwa pamoja,kubadilishana uzoefu, kuwaleta WANAWAKE pamoja na kuimarisha mshikamano wao.
Kongamano hilo la siku moja lilihudhuriwa na wanawake wajasiriamali ,wafanyabiashara,watumishi wa Serikalini,viongozi wa vyama mbali mbali vya siasa , Chama cha Mapinduzi,Taasisi na Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali.
Machi 8 kila Mwaka Duniani kote huazimisha Siku ya Mwanamke Duniani ambapo kilele cha Maadhimisho hayo Ki .Mkoa yatafanyika siku ya Alhamis katika Uwanja wa Samora na Mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Halima Dendego.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa