Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo imewaagiza wawakilishi kutoka Taasisi ya Creative Industry Network Tanzania (CINT) wamefanya kikao na wasanii mbalimbali wa Manispaa ya Iringa kinachohusu mabadiliko ya sheria na kanuni mpya kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Siasa na Kilimo
Kikao hicho kimeendeshwa tarehe 9.01.2021 kwa lengo la kukusanya maoni mbalimbali kutoka kwa wasanii hao pia kuwapa Elimu ya sheria na kanuni zinazowasimamia wasanii
Mgeni rasmi mhe.Richard Kasesala ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa amehudhuria katika kikao hicho na kuwataka wasanii hao kuwa huru kutoa mawazo yao ili kuleta mabadiliko katika tasnia yao ya usanii
Nae, Innocent Nganyagwa, mmoja wa wageni hao amewataka wasanii hao kuzijua sheria ambazo zitawasaidia katika utendaji kazi wao kwa kuzingatia maadili ya kazi
Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Iringa Ndugu, Carlos Mbinda ametoa pongezi na shukrani kwa ugeni huo, kujali wasanii katika uboreshaji tasnia ya Sanaa
Kabla ya mkutano huo, viongozi hao walipata nafasi yakutembelea makundi mbalimbali ya sanaa ndani ya Manispaa kwa dhumuni la kujuzana taratibu za sanaa zinavyotakiwa kuendeshwa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa