Wataalam kutoka Sekretarieti ya Mkoa na Manispaa ya Iringa wameshauriwa kuimarisha mifumo iliyopo katika Sekta za umma kwa kuishirikisha jamii katika masuala mbalimbali ili kuimarisha utawala bora.
Nazar Sola ni Mshauri wa Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Wananchi Mradi wa Uimarishaji mifumo ya sekta za umma PS3+ akitoa mafunzo katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa amesema jukumu lake kubwa ni kujua namna gani mikutano ya kisheria inafanyika, namna ambavyo tovuti za Halmashauri na za Mikoa zinaendeshwa na zitoe taarifa gani kwa wananchi,namna gani matumizi ya mbao za matangazo yanasimamiwa na kuratibiwa na jinsi gani masanduku ya maoni yanaratibiwa.
Aidha Sola amesema Utawala Bora na ushirikishwaji jamii unatekelezwa katika mikoa 13 ambayo ni Kagera,Mwanza,Mara, ,Kigoma,Rukwa,Mbeya, Iringa Shinyanga,Njombe,Dodoma, Morogoro, Lindi na Mtwara ambapo wamebaini mapungufu kidogo ikiwemo kusahaulika kwa wananchi wa hali ya chini kwa kutokushirikishwa katika masuala ya kijamii kutokana na njia zinazotumika kutoa taarifa kutowafikia.
Sola amesema ipo haja ya kuwafikia wananchi hao ambao hawawezi kupata taarifa kupitia Radio,Luninga,au magazeti na wanaoshindwa kufika kwenye mbao za matangazo kwa kuwafata katika maeneo ya mikusanyiko kama vile maeneo ya masoko,vituo vya mabasi,kwenye nyumba za lbada, zahanati, vituo vya afya na Hospitalini kwa kubandika matangazo maeneo hayo kwa lengo la kuwapa taarifa wananchi
Asha Kitegile ni kaimu Mkuu wa Idara ya utawala na Rasilimali watu ameshukuru kwa mafunzo hayo na kuahidi kuyatendea kazi mapungufu yaliyojitokeza kwa manufaa ya Manispaa na jamii kwa ujumla
Mkutano huo wa siku moja umefanyika tarehe 20/7/2021 ambapo umewashirikisha wajumbe kutoka sekretarieti ya Mkoa pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara na vitengo, kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa