Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi,Afya na Elimu Mhe: Eliud Mvela amewataka wataalamu wa Manispaa ya Iringa kuzingatia ubora wakati wa kutekeleza Miradi ya Maendeleo
Mvela amesisitiza kuwa upo umuhimu wa kumaliza kutekeleza miradi hiyo kwa wakati uliopangwa na kuzingatia matumizi sahihi ya fedha zilizotengwa kukamilisha miradi ya maendeleo ili iweze kutatua changamoto za wananchi wa Manispaa
Aidha Mvela ameyasema hayo leo tarehe 4/5/ kwenye Ziara ya robo ya tatu Januari-Marchi 2021 iliyofanywa na kamati ya Uchumi,Afya na Elimu kukagua miradi ya Maendeleo kwa lengo la kuona mafanikio na changamoto zilizopo ili waweze kutafutia ufumbuzi
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo amewapongeza wataalamu kwa kazi nzuri wanayofanya ya ujenzi wa miradi hiyo na kushauri jitihada hizo ziendelee kwani zitasaidia kuiletea maendeleo ya haraka Manispaa hii
Omary Mkangama ni kaimu Mkurugenzi wa Manispaa amesema amepokea maelekezo yote yaliyotolewa na atayafanyia kazi kwa manufaa ya wananchi na Halmashauri kwa ujumla
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na kamati hiyo ni pamoja na Ujenzi wa choo zahanati ya Kitanzini,Ujenzi wa Madarasa shule ya Msingi Maendeleo na Ujenzi wa Kituo cha Afya Mkimbizi.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa