Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uongozi ya Manispaa ambaye ni Meya wa Manispaa Mheshimiwa Alex Kimbe amesema kuwa watendaji na wataalamu wa Manispaa wanatakiwa kusimamia miradi ya maendeleo bila kuchoka kwani kwa kufanya hivyo watatimiza wajibu wao wa kuwahudumia wananchi.
Amesema hayo baada ya kukagua miradi ya maendeleo ya Ujenzi wa Shule ya Mivinjeni, Ujenzi wa jengo la maabara na na Uchuguzi linalojengwa katika hospitali ya frelimo pamoja na ukarabati wa soko kuu la Manispaa.
Amesema miradi mingi inashindwa kukamilika kwa wakati kutokana na wataalamu kutosimamia miradi hiyo ipasavyo, hivyo kufanya miradi mingi kujengwa chini ya kiwango. Amesema miradi iliyokaguliwa ipo katika kiwango kizuri hivyo miradi yote isimamiwe kama ambavyo hii imesimamiwa.
Akichangia katika ziara hiyo Mheshimiwa Frank Nyulusi wa Kata ya Mivinjeni ambaye ni mjumbe wa Kamati ya fedha na Uongozi amesema kuwa ipo haja ya wataalamu muda mwingi kuutumia katika kusimamia miradi kuliko kukaa maofisini kwani kwa kufanya hivyomiradi itatekelezwa kwa wakati na bila malalamiko yoyote.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa