“ Ni marufuku watendaji wa Kata na Mitaa katika Manispaa ya Iringa kujihusisha na uuzwaji wa viwanja katika maeneo yenu au kuwa mashahidi ili kuepuka migogoro ya ardhi katika maeneo yenu.” Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi, Amina Masenza alipokuwa na kikao kazi katika yake na watendaji wa Kata na Mitaa katika ukumbi wa community centre Manispaa ya Iringa.
Amesema migogoro mingi ya ardhi inakuja kugundulika kuwa hata watendaji wa serikali wanahusika kutokana na kuwa mashahidi wa wanao nunua ardhi hivyo kukuza migogoro ya ardhi katika Manispaa ya Iringa.
Amesema watendaji wa kata na Mitaa wanatakiwa kutatua kero za wananchi kwa kufanya mikutano ya hadhara katika Kata na Mitaa yao kwani watendaji wa Kata ndio walinzi wa amani katika kata zao.
“ Migogoro mingi inaweza kutatuliwa ngazi ya Kata ila kwakuwa hamtimizi majukumu yenu na kukwepa majukumu mnawaandikia wananchi barua na kuwaambia waende ngazi ya wilaya wakati uwezo wa kutatua migogolo kwa ngazi ya Kata mnayo.” Kila mmoja atomize wajibu wake.” Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi, Amina Masenza.
Aidha, amewataka watumishi wote ngazi ya kata kuwa na mipango kazi inayotekelezeka na kufanya tathmini ya kazi zao ili kuweza kujipima.
Kikao hicho kimehuhuriwa na viongozi mbalimbali ngazi ya Mkoa, mkurugenzi manispaa, wakuu wa idara pamoja na watendaji wa Kata na watendaji wa mitaa ambapo Manispaa kuna jumla ya mitaa 192.
Habari zaidi tembelea tovuti ya Manispaa
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa