WATOA HUDUMA ZA AFYA BINAFSI WASAINI MkATABA NA MANISPAA YA IRINGA.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndg.Hamid Njovu Pamoja na wamiliki wa Zahanati na vituo vya afya binafsi wamesaini mkataba baina ya serikali na sekta binafsi.
Akizungumza katika tukio hilo Mkurugenzi wa Manispaa Ngd.Hamid Njovu amesema lengo la mikataba hiyo ni kutengeneza ukaribu kati ya watoa huduma na Serikali ambao wote wana jukumu la kuhudumia wananchi katika sekta ya afya.
“huu mkataba utambana yule mtoa huduma kwa sababu kuna vitu tutataka atekeleze kwa mujibu wa sheria na taratibu za afya katika nchi hii, na pia inaisaidia serikali pale ambapo wanataka kutoa misaada katika taasisi hizo kwakupeleka vifaa au watumishi na wataalamu katika vituo vyao”.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa Bi.Jesca Lebba amesema zoezi hilo ni la muhimu sana kwani litasaidia kutoa huduma bora kwa wananchi Pamoja na kurahisisha utekelezaji wa mpango wa afya ya msingi.
“Mikataba hii itaisadia na kuwawezesha hawa wahudumu binafsi kupata rasilimali sababu tutawapelekea vitu mbalimbali kama chanjo, dawa za magonjwa ya moja kwa moja kama kifua kikuu”.
Nao baadhi ya wamiliki na wawakilishi wa vituo vya afya na zahanati wamesema mkataba huo unafaida kubwa sana kwao kwani utasaidia kuongeza wateja pamoja na kufanya kazi kwa ukaribu Zaidi na serikali.
Zoezi hilo limefanyika hii leo katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa, na mikataba hiyo husainiwa kila baada ya miaka mitatu.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa