Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela amewataka watoto wa kike kujitambua na kupata elimu ya ufahamu wa maumbile yao ili kuepuka maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU)
Mh kasesela ametoa wito huo katika siku ya mtoto wa kike duniani iliyofanyika viwanja vya Mwembetogwa Manispaa ya Iringa ambapo amewataka watoto wa kike kuwa na maadili ya kitanzania ili kuepuka maambukizi ya VVU.
Aidha Mh kasesela amesisitiza watoto wa kike kupenda michezo na kuacha tamaa ambazo zitawasababishia kuingia kwenye masuala yasiyofaa na kuwakumbusha kuwa UKIMWI bado ni changamoto katika mkoa wa Iringa na amewahimiza wataalamu wa afya waliopo ndani ya Manispaa ya Iringa kuhakikisha wanawapatia chanjo ya kinga ya saratani ya mlango wa kizazi.
Maadhimisho hayo yameongozwa na kauli mbiu isemayo IMARISHA UWEZO WA MTOTO WA KIKE, na yameandaliwa na Manispaa ya Iringa kwa kushirikiana na Taasisi ya mikopo Iringa (BRAC) pamoja na shirika la IDYDC.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa